Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewataka watendaji kuhudhuria vikao kwa lengo la kutatua changamoto zilizopo katika Kata.
Ngwada amesema hayo katika Mkutano wa Baraza la kupokea Taarifa kutoka kwenye Kata kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024 uliofanyika Novemba 13, 2023 katika Ukumbi wa Manispaa.
“Kikao hiki ni muhimu kwasababu kinaleta changamoto zilizopo katika Kata zetu, hivyo naagiza kufuatiliwa kwa Ujenzi wa Shule ya Mchepuo wa Kiingereza(English Medium)” Amesema Ngwada
Ameongeza kwa kusema Shule hiyo ina thamani kutokana na unafuu wa gharama na italeta heshima kwa Kata na Manispaa kwa ujumla lakini isipotekelezeka basi heshima itakuwa imevyunjwa.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Julius Sawani amepongeza jitihada zilizoonyeshwa katika mradi wa Community Center na Tembo Bar kwa hatua waliyofikia na kuwasisitiza kuwa watekeleze kufuatana na makubaliano yalivyokuwa katika vikao vilivyopita na sio vinginevyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala amesisitiza juu ya utekelezwaji wa miradi iliyopo katika bajeti.
“Tufanye zaidi marejeo ya bajeti zetu tukusanye pesa na zipelekwe kutekeleza miradi iliyopo katika bajeti na tusilete kitu kipya ambacho hakikuwepo kwenye bajeti kwani kitatusumbua katika utekelezaji” Amesema Msigala
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa