WATUMISHI katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wametakiwa kuboresha utendaji wao wa kazi ili kuiletea maendeleo halmashairi hiyo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada, alisema hayo Februari 12, 2022 kwenye sherehe za watumishi wa Manispaa hiyo za kuukaribisha mwaka 2022 ambazo zimekuwa zikifanyika kila mwaka.
Mhe Ngwada alisema yeye pamoja na madiwani wenzake watawaunga mkono na kutoa ushirikiano kwa watumishi hao ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi mkubwa.
"Mwaka jana 2021 Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilifanya vizuri sana katika mashindano ya usafi wa mazingira na kushika nafasi ya pili kitaifa hii inaonyesha ni namna gani tunavyoshirikiana sisi madiwani na wataalam," alisema Mhe. Ngwada.
Aidha, Mhe. Ngwada amewashukuru watumishi hao kwa ushirikiano mzuri baina yao na Baraza la Madiwani kwa ujumla kwa kipindi alichoingia madarakani mpaka sasa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg. Gerald Mwamuhamila amewapongeza watumishi kwa jitihada za utendaji kazi wao katika kila nyanja na kuwaomba waendelee kuwa na moyo wa kizalendo katika kudumisha amani, kuwajibika katika kuleta maendeleo ndani ya Manispaa ya Iringa.
Awali akitoa zawadi kwa Mstahiki Meya pamoja na Mkurugenzi Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ndugu Mlole Ngwada aliwashukuru wajumbe kwa ushirikiano na kukabidhi zawadi ya kalenda ya Mwaka 2022 kwa Mstahiki Meya yenye picha mbalimbali ambazo zinaonyesha Mstahiki Meya akishirikiana na wananchi katika shughuli za maendeleo.
Mlole pia alikabidhi zawadi ya bango linaloonyesha picha mbalimbali za miradi ya maendeleo iliyotelelezwa na Halmashauri kwa kaimu Mkurugenzi.
Aidha sherehe hizo zilizohudhuriwa na watumishi wa kada mbalimbali pamoja na Baraza la Madiwani zilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo muziki wa dansi (live band) ambapo walipata fursa ya kuselebuka kwa pamoja.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa