Kikao hiki cha siku moja kimefanyika leo tarehe 13/12/2022 kimewahusisha wakuu wa Sehemu na vitengo na watumishi wa kada zote waliopo ofisi kuu.
Akiongea katika kikao hiki Mhe.Ngwada amesema ni vyema watumishi wote wakapata stahiki zao kwa wakati na kuzingatia usawa katika utoaji wa malipo ya watumishi wote bila kujali nafasi zao za kazi.
'Niseme hivi anayestahili kulipwa pesa kutoka katika nafasi yeyote aliyoko haijalishi ni mhudumu ama ni afisa alipwe na kusiwe na ubaguzi wakati wa malipo alisema Ngwada'
Pia Mstahiki Meya amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa aepuke kufanya matumizi yasiyo kuwa katika bajeti ili kuepuka hoja za ukaguzi .
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr.Stephen Ngwale amesema ameyapokea maelekezo yote na atayafanyia kazi na kuwataka wakuu wa Sehemu na vitengo kufanya vikao vya ndani ambavyo vitapunguza changamoto zinazojitokeza katika Sehemu na Idara zao.
Naye mhe.Juli Sawani naibu Meya wa Manispaa ya Iringa amewataka wakuu wa Idara na vitengo kuwa wa wazi na mahusiano mazuri na watumishi wa chini kwani kufanya hivyo itasaidia kupunguza malalamiko
Kwa upande wake paul Mpwehe Mtumishi kutoka Sehemu ya Maendeleo ya jamii amesema kuwa amefurahishwa sana na kukao hicho na kuongeza kuwa ni utamaduni mzuri ambao unaleta uwazi kwani unaondoa kero za watumishi hivvyo kuwafanya wawe na utulivu katika maeneo ya kazi na kuwa na morali ya kazi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa