Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr.Jesca Lebba amewataka wanawake vinara wa lishe kuhakikisha wanatoa Elimu ya mlo kamili
ili Kuketa mabadiliko katika jamii.
Dr.Lebba ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Hall mark kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa wakati akifungua semina ya siku moja iliyowashirikisha wahudumu wa afya katika ngazi ya jamii pamoja na baadhi ya wataalamu wa lishe ngazi ya Halimashauri pamoja na ofisi ya mkuu wa Mkoa.
Dr.Lebba amesema bado wanawake vinara wanao wajibu wa kuelimisha jamii kuanzia katika ngazi ya familia kuhusu mlo kamili na kuwa wao ndio wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa wanatakiwa kuhakikisha jamii inajenga utamaduni wa kula makundi matano ya vyakula ili kuhakikisha wanatokomeza tatizo la udumavu na utapiamlo.
Dr.Lebba anashangazwa na takwimu za utapiamlo katika Mkoa wa Iringa kuwa ni asilimia 47 na kuwa Mkoa unaongoza kwa kushika nafasi ya pili kitaifa ilihali uzalishaji wa mazao ya chakula ni wa kiwango cha juu.
Akitoa mada katika mafunzo hayo Afisa lishe Manispaa ya Iringa Bi.Anzael Msigwa amesema ni vyema kina mama wajawazito kuhakikisha wanawahi kuanza clinic mapema kabla ya miezi mitatu ili kunusuru afya ya mtoto na udumavu pamoja na magonjwa mengine.
Msigwa anasema ni vema mtoto apate vichanganshi tangu akiwa mdogo ,pamoja na mama mjamzito kula mlo kamili,na kupata huduma za awali toka kwa wataalam pindi anapowahi kuanza clinic kwani kwa kufanya hivyo Itasaidia sana mama mjamzito kujifungua mtoto mwenye afya njema .
Happiness Siliwa muwezeshaji kutoka lishe endelevu anasema mradi huu wa miaka mitano umumefadhiliwa na USAID kwa kushirikiana na wadau wengine kama Deloit,African Academy, na Save the Children unafanya kazi katika Mikoa minne ambayo ni Iringa,Dodoma,Morogoro na Rukwa,na umepanga kuwafikia wanawake wapatao milioni moja na laki tano,vijana pamoja na watoto.
Mafunzo hayo yenye jumla ya washiriki thelasini yamefunguliwa na kufungwa na Mgeni rasmi Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa