• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

MGOGORO WA BAJAJI NA DALADALA MANISPAA YA IRINGA KUPATIWA SULUHU

Posted on: April 28th, 2021

MAAZIMIO YA UTARATIBU  WA BAJAJI NA DALADALA KATIKA MANISPAA YA IRINGA KUTOKANA NA UAMUZI WA BARAZA MAALUM LA MADIWANI LILILOKAA TAREHE 28.04.2021

Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imepitia changamoto na migogoro mingi ya vyombo vya usafirishaji katika mji wetu. Migogoro hiyo imesababisha kuwepo kwa migomo ya mara kwa mara kwa madereva wa bajaji na daladala hivyo kuhatarisha usalama na kuondoa hali ya utulivu katika Manispaa yetu. Vikao na mikutano mbalimbali vilifanyika na mapendekezo mbalimbali yaliwasilishwa ili kuweza kutatua changamoto hizo.

Baraza Maalum la Madiwani limekaa tarehe 28.04.2021 kujadili changamoto hizo na kutoa maamuzi yafuatayo:-

  • Bajaji zote za zamani zinazotoka nje ya Mkoa wa Iringa hazitapokelewa na kupewa namba ya usajili. Aidha bajaji zitakazopokelewa na kusajiliwa ni bajaji mpya na zitapangiwa vituo vya  pembezoni mwa Mji.
  • Bajaji zote zitapangwa katika vituo maalum na kwa kuzingatia ukanda wake   
  •          (zone).
  • Bajaji kwa kila kanda (zone) zitakuwa na idadi maalum kulingana na mahitaji.
  • Kamati  Maalum ya Madiwani imeamua kuwa:-
  • Eneo la Stendi ya Miyomboni litumike kwa bajaji za Kihesa na Ipogolo na daladala zilizokuwa zinatumia stendi ya Miyomboni zitumie Stendi Kuu ya Zamani.
  • Bajaji za Don Bosco, Mtwivila, Mawelewele, Mkwawa zitatumia kituo cha barabara mbili.
  • Bajaji zote za ukanda wa Kihesa na Mkimbizi hazitaruhusiwa kupita barabara kuu ya Dodoma kuanzia mnara wa saa wa Manispaa na badala yake zitapitia barabara ya Mama Siyovelwa (Mahatmaghand) kupitia Shule Sekondari ya Wasichana Iringa hadi  Transforma Kihesa kwenda Ngome Shule ya Msingi.
  •  Ambapo Bajaji za Mkimbizi zitavuka kupitia njia ya Ngome Shule ya Msingi kwenda Mwang’ingo na kuvuka barabara kuu kwenda Mkimbizi.
  • Bajaji za Kihesa zitaendelea kwa kupitia Hospitali ya Ngome kwenda Kihesa Sekondari na Chuo Kikuu cha Tumaini.
  • Bajaji za Nduli na Kihesa Kilolo zitapita njia ya Mkimbizi kutokea Bwawani na kuendelea na barabara kuu ya Dodoma Road.
  • Bajaji zote za ukanda wa Ipogolo zimeruhusiwa kupandisha juu kupitia barabara kuu kwa kukatishi kwa Mambo kupitia barabara ya Legezamwendo na shooters kuishia Stendi ya Miyomboni.
  • Bajaji za Isakalilo zitapitia zizi kwenda pembezoni kote na hazitapandisha kupitia barabara ya zizi kona ya kabari kwenda Mlandege.
  •  
  • Bajaji za Isakalilo kama zitataka kwenda na kutoka mjini zitatumia
  • Njia ya Kwakilosa kupitia Don – Bosco na kuishia kituo cha barabara mbili.
  • AU
  • Bajaji zitapita barabara ya Kihodombi, Mwangata, Machinjio ya Mlandege kutokea Kijiweni soko la Samaki, njia ya Holiday kupitia Msikiti wa Hidaya na kwenda Mashine tatu.
  • AU
  • Bajaji zipite Njia ya Mashine tatu kupitia msikiti wa Hidaya kwenda kukatishia soko la Samaki Kijiweni kwenda Machinjio ya Mlandege hadi kona ya Kabari na kutelemkia kwenda njia ya Mwalugenge (kulia) kwenda Zizi.
  • Bajaji zote haziruhusiwi kupita barabaza zote zilizoandikwa No. Entry.  Barabara hizo ni Pamoja na:-
  • Barabara ya kuanzia mnara wa  saa kwenda Kihesa.
  • Barabara ya Mwang’ingo kuja Mjini na Mwang’ingo kwenda TRM
  • barabara ya njiapanda ya Mtwivila kwenda Mjini na kwenda Mwang’ingo.
  • Barabara za kwenda stendi kuu ya zamani, ambazo ni njia ya Zebra kwenda Stendi kuu ya zamani, Mashine tatu kwenda stendi kuu ya zamani, barabara ya mzunguko wa stendi kuu ya zamani na njia ya Mwembetogwa kuingia stendi kuu ya zamani, njia ya MR Kwenda stendi kuu ya zamani na Njia ya kutokea magari yanatotoka stendi kuu ya zamani.
  • Barabara ya kuanzia Zebra kuu (VODASHOP) hadi Samora.
  • Daladala za Tumaini zitaishia Kigonzile shule ya Msingi na sio Tumaini Chuo kama ilivyokuwa awali.
  • Bajaji za Frelimo zitaishia Kituo cha Mashine tatu.
  • Bajaji za Mtwivila zitapitia njia ya Chuo Kikuu cha Mkwawa kwenda na kutoka Mtwivila na njia ya Magic Site kwa kupitia Mkwawa Sekondari.
  • Ili kuhudumia wananchi wa Kihodombi itarudishwa route ya daladala ya Kihodombi Tumaini.
  • Route zote za daladala zirudi na kuanza kufanya kazi kama ilivyokuwa awali Pamoja na marekebisho yake katika maeneo hayo.
  • Vituo vya Soko Kuu na Shooters Pamoja na MR vilivyokuwa vinatumiwa kama stendi ya Bajaji vimefutwa.

Maazimio hayo yamepitishwa na kuthibitishwa na Mkutano Maalum wa Baraza la Madiwani uliokaa tarehe 28.04.2021.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUCHUKUA FOMU YA UJENZI WA JENGO LA BIASHARA TEMBO BAR February 15, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, 2023/2024 July 13, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI July 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 23, 2024
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • PPP CENTRE YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU IRINGA MC

    April 04, 2025
  • ALUTE: "HAKIKISHENI MIRADI INAKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA"

    December 21, 2024
  • UCHAGUZI HURU NA WA HAKI UNAHITAJI USHIRIKISHAJI - RC SERUKAMBA

    October 10, 2024
  • MSIGALA AWAONYA MAAFISA MAENDELEO KUJIHUSISHA NA MIKOPO HEWA

    October 05, 2024
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA,2023/2024
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa