Picha ikiwaonesha baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wote wa Mkoa wa Iringa waliohudhuria katika mkutano wa Mlezi wa Chamà Cha Mapinduzi Mh. Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya Nne Mh. Mizengo Peter Kayanza Pinda ambaye pia ni Mlezi wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa Iringa amekutana na kuzungumza na Wabunge pamoja Madiwani wote wa Mkoa wa Iringa kuhusiana namna na utekelezaji wa majukumu yao hasa Ilani ya CCM, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano CCM Mkoa leo Tarehe. 13.01.2021
"Hata hivyo utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa miaka mitano iliyopita chini ya Rais wangu Magufuli umetusaidia sana nchini kwetu hadi tulipo fikia hvyo basi hata nyie mnatakiwa kwenda kufanyika kazi ili ifikapo mwaka 2025 tusihangaike kuzitafuta kura"
Aidha ikumbukwe kuwa Mkoa wa Iringa umefanikiwa kuwa na Wabunge wote na Madiwani wote waliochaguliwa na wananchi kutoka chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa 2020
Pia Mh. Pinda amewaonya viongozi hao kutobaki na makundi ya kipindi cha uchaguzi hivyo kuziunganisha nguvu zao kwa pamoja na kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi na wananchi kwa uzalendo
"Rushwa tuipinge jamani, tufanye kazi kwa kuzilinda haki za wananchi hivyo wewe kama Mbunge au Diwani unapaswa kupinga rushwa yaani usipokee wala usitoe rushwa" Mh. Pinda alisema hayo
Kwa upande mwingine Mh. Pinda amewataka viongozi hao kujenga mahusiano mazuri ndani ya Jimbo na kata kwa watumishi wenzao na sio kujiona ni bora zaidi, huku akihamasisha kuyatunza mazingira pamoja na kujitegemeza kimapato ndani ya chama
Hata hivyo Mh. Pinda amewaamuru viongozi hao kujiwekea utaratibu wa kwenda kukagua miradi mbalimbali inayofanyika katika Halmashauri zao kwa kuangalia kama Ilani iliyonadiwa kipindi cha Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ya Chama Cha Mapinduzi inavyotekelezwa
Hata hivyo Mh. Pinda ametoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kuendelea kuzitambua na kuzisaidia sekta binafsi katika shughuli zao kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa serikali kupitia ulipaji wao wa kodi na tozo zote kwa kiserikali
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ally Hapi amemshukuru Mh. Pinda kwa ujio wake wa kuja kukutana na viongozi hao huku akiwomba wabunge kuwatumikia wananchi kwani nguvu kubwa ya ushindi wao imetokana na Madiwani hao
Saidi Rubeya ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa amewashukuru viongozi wote waliofika kikaoni hapo na kuwaomba kwenda kuyatendea kazi yote waliyoelekezwa
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu, Dr. Abel Nyamahanga amewatakia utekelezaji mwema wa Ilani ya Chama Cha Mapindzi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa