Wataalamu katika sekta mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wameaswa kutambua dhamana ya uongozi wao ni kuwatumikia watanzania kwa kuhakikisha wanaleta maendeleo chanya katika jamii.
Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge-TAMISEMI Mhe. Dennis Londo wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Iringa uliofanyika Oktoba10, 2023.
Mhe.Londo amewapongeza wataalamu wote kwa juhudi waliyoionyesha katika kukamilisha miradi muhimu ndani ya Manispaa na kuwaasa kukumbuka dhamana ya uongozi wao nikuwatumikia watanzania.
“Tumekagua miradi yote kuanzia Soko la Mlandege (Mwamwindi), Stendi ya Igumbilo na barabara ya kutoka Don Bosco kuelekea Mawelewele hakika niwapongeze, pia nahitaji Wataalamu wote watambue dhamana ambayo wamepewa na watanzania wote nikupanua miundombinu, kuongeza tija na kuhakikisha mapato ya Serikali yanaongezeka”Amesema Mhe. Londo
Mhe.Londo ameongeza kwa kusema kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge-TAMISEMI imegundua ujenzi wa jengo la utawala haukuzingatia viwango.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuzidi kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya ULGSP zaidi ya Tsh. Bilioni 23 kwa mwaka wa fedha 2013/2014-2017/2018 na kisha kuongezewa muda hadi mwaka 2019/2020 kwaajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo; Ujenzi wa barabara ya Samora kuelekea Mashine tatu mpaka Frelimo, Ujenzi wa barabara ya Don Bosco kuelekea Mawelewale kwa kiwango cha lami Kilomita 2.8 kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri”
Aidha Ndg. Msigala ameendelea kusema Ujenzi wa Soko la kisasa la Mlandege umegharimu Tsh.Bilioni 3.7, Ujenzi wa Stendi Kuu ya Igumbilo ambayo inauwezo wa kupokea mabasi 60 na magari madogo 20 ambapo kwa siku inapokea magari 200 na miradi mingine.
Mkuuw a Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge-TAMISEMI na kuahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo na kutoa taarifa ya utekelezaji kila robo ya mwaka wa fedha kwenyekamati hiyo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa