Kaimu mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Pololet kamando Mgema amefurahiswa na ubunifu uliofanywa na wakulima,wafugaji na wavuvi wa Manispaa ya Iringa katika maonesho ya nanenane 2022 yanayofanyika kitaifa Jijini Mbeya.
'Nimefurahishwa sana na ubunifu wa hali ya juu mliofanya katika maonesho haya mna bidhaa nzuri zenye ubora, uwepo wa shamba darasa la parachichi inaleta hamasa kwa jamii kuja kwa wingi kujifunza kilimo hicho hakika Manispaa ya Iringa mko juu alisema Mgema'
Mhe.Mgema amesema hayo leo tarehe 5/8/2022 alipokuwa akitembelea banda la Manispaa ya Iringa ikiwa ni utaratibu uliowekwa viongozi mbalimbali kutembelea mabanda ya maonesho ya nane nane kila siku.
Dr.Stephen Ngwale ni Mkuu wa Idara ya mifugo na uvuvi Manispaa ya Iringa amesema Manispaa ya Iringa ni miongoni mwa Halmashauri,taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za kiserikali ambazo zinashiriki maonesho ya nanenane kitaifa Jijini Mbeya,katika ushiriki huo Manispaa imefanikiwa kuwawezesha wakulima na wafugaji hamsini na saba (57 )pamoja na wataalam kumi na sita (16) kushiriki maonesho hayo kwa lengo la kujifunza,kutoa elimu, na kushindana ngazi ya kanda na kitaifa kwa kuzingatia kauli mbiu Ajenda 10/30 Kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi.
Aidha maonesho ya nane nane 2022 kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya ambapo yalianza tarehe 1 agosti na yatamalizika tarehe 8 Agosti mwaka huu .
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa