Ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara yenye kauli mbiu “Amani na Umoja ni nguzo ya Maedeleo yetu” Wilaya ya Iringa imefanya kongamano la kujadili Maendeleo ya miaka 61 ya Uhuru leo 9 Disemba 2022 katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo Manispaa ya Iringa.
Akizungumza katia kongamano hilo Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Mohamed Moyo amesema kuwa tulipo toka na tulipo sasa hivi kama nchi tumepiga hatua kubwa sana kwa kuwa Sekta zote za ,kiuchumi, na kijamii kuna mabadiliko makubwa hususani kwa mtu mmoja mmoja.
Moyo amesema kuwa ni lazima watanzania wajikite katika maendeleo ili kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini lakini bila kusahau uzalendo kwa kuwa ndio kitu kikubwa.
Awali akiwasilisha mada katika kongamano hilo Mhadhiri kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii CDTI Musa Rashid amesema kama Nchi mpaka sasa imefanikiwa kuhakikisha inapambana na ujinga umasikini na maradhi kwa kuanzisha shule,,kufungua vituo vya Afya na kutoa Mikopo isiyo na riba kwa wananchi kwa lengo la kuwainua kiuchumi
“Tumefanikiwa kupambana na ujinga kwa kuwa shule zimejengwa kila sehemu hakuna mahali ambapo hakuna shule hilo limetusaidia kupiga hatua kwenye Sekta ya Elimu”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kupinga ukatili Mkoa wa Iringa nduguu Silvano Ernest amesema kuwa kupitia Maadhimisho hayo ya miaka 61 ya Uhuru yaende sambamba na kupinga ukatili kwa watoto na wanawake ili kukomesha matendo hayo katika jamii yetu.
Naye mwananfunzi kutoka Chuo Kikuu cha Katholiki ( RUCU) ndg.Desmond Laurent amesema kuna haja ya kuendelea kuwa na makongamano kama hayo kwakuwa yanaendelea kutukumbusha watanzania thamani ya kuendelea kulinda Uhuru wa Taifa letu.
Mada zilizowasilishwa katika kongamano hilo ni Maendeleo endelevu ya Elimu,Maendeleo ya jamii katika nyanja zote,,uzalendo na mchango wa viongozi katika harakati za ukombozi.
Akifunga kongamano hilo Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo amewataka watanzania wote kuendelea kudumisha uhuru na kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kwani hiyo ndiyo zawadi pekee tuliyopewa na waasisi wa Taifa letu.
Aidha Mhe Moyo amekemea tabia ya baadhi ya watu kutumia vibaya jukwaa la kisiasa kuwagawa watanzania na kuwataka watanzania wasikubali kugawanywa.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa dini,viongozi wa chama na Serikali,wakuu wa sehemu na Vitengo,watumishi,wanafunzi wa shule za Msingi,Sekondari,vyuo vya kati na vyuo vikuu ambapo awali katika wiki ya maadhimisho hayo shughuli mbali mbali za kijamii zilifanyika.
Shughuli zilizofanyika ni kupanda miti katika shule ya Sekondari ya Mawelewele ,Hospitali ya wilaya ya Frelimo.kufanya usafi na kuona wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa,Mabonanza ya michezo na mashindano ya Insha katika Shule za Msingi na Sekondari ambapo washindi walikabidhiwa zawadi na Mgeni rasmi katka kilele cha Maadhimisho hayo.
K/Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Manispaa, Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa