Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Halima Dendego amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi katika Kata ya Kitwiru na Kata ya Mwangata sambamba na kuacha maagizo kwa viongozi na wataalamu.
Amekagua miradi hiyo akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Mhe. Veronica Kessy, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada, Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastory Msigala, Wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Kitwiru, Ofisi na matundu ya vyoo uliogharimu Tsh. Milioni 347, ujenzi wa Shule ya Sekondari iliyopo eneo la Kilongaena uliogharimu Tsh. Milioni 583 na kufikia 58% mpaka sasa na kumaliza ziara yake kwa kutembelea ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Mawelewele unaogharimu Tsh. Milioni 130.
Mheshimiwa Dendego amewashukuru wasimamizi wa miradi yote kwa kusimamia vyema na kutoa maagizo ikiwa ni pamoja na kuwekwa kwa umeme katika Shule hiyo ya Msingi pamoja na kufanyiwa usajili ili ianze matumizi mapema na kuepusha tatizo la watoto kusoma mbali.
Aidha Mhe. Dendego ametuma shukrani zake kwa Bwana Daudi Kwavava aliyetoa eneo lake ili kujengwa kwa Shule ya Sekondari
“Kwa kweli tunamshukuru Bwana Daudi Kwavava na mfikishieni salamu sisi hatuna cha kumlipa lakini tunarudisha fadhila kwa shule hii kupewa jina lake nataka litengenezwe bango zuri sana na kubwa lenye jina lake na nilikute hapa”.
Pia Mhe. Dendego ameagiza barabara inayoelekea shuleni hapo kurekebishwa kwa kiwango cha lami na kuahidi kukagua shule hiyo mwezi wa kumi na moja mwanzoni.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa