Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa ndugu Abel Nyamahanga amekemea vikali tabia ya baadhi ya watia nia wa nafasi ya ubunge kupitia chama hicho kujipitisha kwa wanachama na kutoa rushwa kwa lengo la kujiwekea mazingira mazuri ya kupitishwa wakati wa mchakato wa kura za maoni.
Nyamahanga amesema hayo katika kikao chake na wanahabari mkoa wa Iringa, kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa Leo.
" tutachukua hatua kali dhidi ya mwanachama yoyoye atakaebainika kutoa au kupokea rushwa. Nyamahanga aliongezea
Aidha Nyamahanga ametoa onyo kwa viongozi wa chama wenye dhamana ya kusimamia uchaguzi kutopendelea mgombea au mtia nia yeyote kwa lengo la kutaka ashinde.
Naye mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (MNEC) ndg Salim Abri amesema chama Cha mapinduzi kiko imara na wamejidhatiti kumsimamisha mgombea mwenye sifa.
Ameongeza kuwa ana uhakika wa ushindi wa kishindo kupitia chama Cha Mapinduzi .
Akijibu swali la mwandishi wa habari juu ya MNEC huyu kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini, amesema kuwa Ccm ina wanachama madhubuti na wenye sifa hivyo chama hakiwezi kukosa mgombea na sio lazima yeye agombee nafasi hiyo.
Amesema ana imani na mgombea atakayepitishwa na Ccm katika kinyang'anyiro hiko.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa