Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahimu Ngwada ameutangazia umma juu ya kununuliwa kwa Timu ya mpira wa miguu ya Ruvu Shooting na kuwa timu ya Mkoa ikichukua nafasi ya Lipuli FC.
Amethibitisha hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari ofisini kwake Agosti 29, 2023, kuwa wadau wa mpira wa miguu ndani ya Mkoa wa Iringa wameinunua timu hiyo kwa lengo la kuinua vipaji na uchumi wa Mkoa.
“Ni rasmi sasa tumekwisha nunua Timu ya mpira wa miguu ya Ruvu Shooting na kuipa hadhi na jina la timu yetu ya LIPULI FC, hii ni baaada ya majadiliano baina ya viongozi wa timu hizi mbili yaani Lipili FC na African Wanderers FC, Chama cha Mpira wa miguu Mkoa na Wilaya na kufikia makubaliano haya na pia niwaombe wanairinga kuzishika mkono timu hizi mbili kwani tunatamani wananchi wetu wapate burudani ya mpira.”Amesema Ngwada
Aidha Mstahiki Meya amewaasa viongozi wa timu hizo kufanya kazi ili kuhakikisha timu haishuki thamani na kujiepusha na migogoro kwani yeyote atakayekuwa sababu ya migogoro kati ya timu hizo mbili hatoweza kuvumiliwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa