Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg Hamid Njovu, amewataka walimu wote wa shule za Sekondari zilizopo Manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa weledi ili kuchochea maendeleo ya kielimu , ameyasema hayo katika ukumbi wa Lugalo jana ,Katika kikao cha walimu kilifanyika kwa lengo la kuboresha taaluma na kusikiliza changamoto za walimu pamoja na kuzitolea ufafanuzi. Amesema tatizo la kuchelewa kwa baadhi ya walimu kupanda daraja linashugulikiwa kwani utaratibu wa kupandisha madaraja unafanyika kila mwaka na kuwa walimu wanaongezeka kila mwaka,hivyo walimu wawe wavumilivukwani serikali inashughulikia suala hilo.
Kwa upande wake afisa elimu sekondari Tupe kainga,amesema mikakati waliyonayo katika kuhakikisha wanaboresha taaluma ni kuhakikisha wanaongeza ufaulu kwa wanafunzi na kutatua changamoto za wanafunzi kwa kuhakikisha shule zote za Manispaa wanafunzi wanapata chakula cha mchana ili waweze kuwa na usikivu,pia kuhakikisha changamoto zinazowakabili walimu zinatafutiwa ufumbuzi wa haraka ili kuwafanya waweze kufundisha kwa ufanisi.
Bestnest Mwakakamale ni mwalimu wa shule ya sekondari Lugalo Amekiri kuwa kuwepo kwa changamoto ambazo zinapelekea wanafunzi kutokufanya vizuri na kuwa hali hiyo inasababishwa na baadhi ya walimu kutokuwa vizuri kiuchumi, kwani wana madeni mengi kutokana na mishahara kutokupanda kwa muda, pia walimu wengi hawajapanda madaraja kwa muda mrefu hii inapelekea kushindwa kufanya vizuri katika majukumu yao.
Aidha Mwakakamale amesema sababu nyingine inayofanya wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo yao ni kuanza mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni hivyo kushindwa kuzingatia masomo hivyo amewaomba wazazi kufatilia nyendo za wanafunzi hao kwa ukaribu ili wazingatie masomo kwani ndio msingi wa maisha yao ya badae.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa