Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu amefanya kikao na wenyeviti wa mitaa, watendaji wa kata pamoja na watendaji wa mitaa wa Manispaa ya Iringa lengo likiwa ni kuwakumbusha kuhusu Utawala bora, ulinzi na usalama pamoja na kuitambulisha sheria ndogo ya Manispaa ya usafi wa mazingira( ada ya taka).
Akizungumza katika ukumbi wa community centre Ndugu Hamid Njovu amesema kuwa sheria hii ilikuwepo sasa itaanza kutekelezwa ambapo wananchi wa Manispaa ya Iringa watatakiwa kuchangia uzoaji wa taka ambao utakusanywa na watendaji wa mitaa kwa kila kaya kwa mwezi mala moja.
Amesema kuwa viongozi ambao ni wenyeviti wa mitaa ni watu wakubwa na viongozi katika maeneo yao, hivyo ni vyema kila kiongozi akiwa katika eneo lake basi ajitahidi kuacha alama ili hata wakija viongozi wengine baada yake basi kuwe kuna jambo kubwa linalooneka lilifanyika na kiongozi aliyepita na litabaki kuwa kumbukumbu muhimu kwa jamii na serikali.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na wakuu wa Idara mbalimbali za Manispaa ambapo mada ya Afya, elimu na ukusanyaji wa mapato ilitolewa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa