Mkurugenzi wa Halimashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu amewataka watumishi kutojiingiza kwenye makosa ya jinai kwani wanapofanya hivyo wanampa wakati mgumu kama mwajiri
Njovu amesema kuna baadhi ya watumishi wamekuwa watovu wa nidhamu kwa kujiingiza katika makosa ya jinai na wengine wamekuwa wakilewa kupindukia jambo ambalo linaleta sifa mbaya kwa mtumishi wa umma.
Aidha Njovu amesema lengo la mtandao huo ni kuunga mkono juhudi za serikali iliyopo madarakani inayo ongozwa na mh.Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli hivyo ni jukumu lake kama mwajiri kuwafata watumishi wake na kuwapa uwanja mpana wa kueleza changamoto zao na kuona namna ya kuzitatua ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Omari Mkangama ni Afisa utumishi Manispaa ameelezea haki za mtumishi na kusema kuwa mtumishi ana haki ya kwenda likizo,anahaki ya kuomba uhamisho ana haki ya kupata stahiki zake mbali mbali ili mradi tu afuate kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Pia amewataka watumishi kufuata taratibu na kanuni pindi wanapokuwa na madai au maombi kwani baadhi yao wamekuwa wakiruka ngazi jambo ambalo linakiuka kanuni na taratibu zilizo wekwa.
Mwisho wajumbe walipata fursa ya kutoa kero zao ambapo baadhi walijikita katika maeneo ya kutoku panda madaraja kwa muda mrefu ilihali wanasifa,kutokulipwa stahiki zao kama malipo ya kuhama,malipo ya likizo.nk.
Akijibu kero hizo,Mkurugenzi Hamid njovu aliahidi kuzishughulikia .pia mesema ataandaa kikao cha watumishi wote pamoja na wakuu wa idara ili waweze kukosoana ana kwa ana,kwani njia hii itasaidia kupunguza kero zisizo za lazima.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa