"Maombi yenu yote nimeyachukua na naahidi kuyafanyia kazi ndani ya miezi miezi miwili, likiwemo suala la malimbikizo ya fedha za likizo na on call allowance."
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu alipokuwa akizungumza na watumishi wa hospitali ya frelimo katika Manispaa ya Iringa.
Amesema Serikali inathamini sana mchango wa watumishi wa afya, ndio maana maslahi ya watumishi hao lazima yachukuliwe kwa umakini mkubwa kwani ni watu wanaowajibika moja kwa moja na afya za wananchi wengi.
Ameahidi kuboresha huduma kwa kutafuta vifaa vya hospitali ikiwemo kununua utra sound mashine, na mashine za idara mbalimbali zikiwemo za idara ya upasuaji na idara ya meno.
Aidha amewataka makatibu wa Afya kuhakikisha wanakuwa daraja kati ya watumishi hao wa afya na ofisi ya mkurugenzi ili matatizo ya watumishi yasikae muda mrefu bila kushughulikiwa kwani kwa kukaa muda mrafu kunafanya kuzaliwa kwa manun'guniko na hivyo utendaji wa kazi wa watumishi hao wa afya kushuka.
Ndugu Njovu amesema malalamiko yote ambayo yapo ndani ya uwezo wake yatashughulikiwa ndani ya miezi miwili hivyo kuwaomba watumishi hao kufanya kazi kwa kujituma na hari mpya kwani serikali inawategemea kwa kiasi kikubwa ndio maana miundombinu ya hospitali inazidi kuboreshwa ili kuwa maeneo bora ya kufanyia kazi na kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa