Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Hamid Njovu leo amefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2015-2020 katika Halmshauri ikiwa ni mafanikio ya serikali ya awamu ya tano chini ya jemedari Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli.
Njovu amesema lengo la ziara hiyo ni kuwaonyesha kwa vitendo wanahabari pamoja na umma namna ambavyo serikali inawajali wananchi wake na kuwajengea miradi hiyo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,Elimu,Kilimo na mifugo,ujenzi,utawala,biashara maendeleo ya jamii na Maji.
Miradi iliyotembelewa leo ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya mwalimu kigonzile shule ya msingi,ujenzi wa vyumba vya madarasa Mtwivila shule ya msingi,ujenzi wa vyumba vya madarasa na bweni Iringa girls,ukarabati wa Lugalo sekondari,ujenzi wa jengo la uchunguzi Hospitali ya Frelimo, na ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Isakalilo.
Awali akiongea katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard ksesela amempongeza Mkurugenzi Kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia miradi hiyo yenye ubora na ambayo imeleta tija kwa wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Ziara hiyo ya siku mbili imeanza leo 18/8 na itamalizika kesho tarehe 19/8 mwaka huu na imewashirikisha Waandishi wa habari Ishirini na tano kutoka vyombo mbalimbali vya habari,pamoja viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo wakuu wa Idara na vitengo kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa