Mkurugezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Hamid Njovu amehairisha kikao cha Baraza la Madiwani lililopaswa kufanyika leo katika ukumbi wa Manispaa kwa lengo kubwa la kupitia taarifa za robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 kutokana na akidi ya wajumbe kutotimia katika kikao hicho.
“Kwa mujibu wa kanuni namba 9 kifungu cha 4 nina mamlaka ya kuhairisha mkutano huu na nitauitisha tena baada ya siku saba ili kufanyika tena” amesema Njovu.
Aidha akizungumza na wanahabari katika kikao kifupi amesema kuwa, kitendo hicho kimeleta athari katika utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ikiwemo upotevu wa muda pamoja na fedha ambazo zimetumika katika kuandaa kikao hicho.
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa Ndg. Saidi Rubeya katika mkutano wake na waandishi wa Habari ameeleza kuwa Madiwani wa Chama cha Mapinduzi wako sahihi kabisa kugoma kuhudhuria katika kikao cha baraza,amesema sababu za msingi zilizozungumzwa na madiwani kwa uwongozi wa chama, zimeonyesha dhahiri kuwa madiwani hao wakosahihi kutokuhudhuria katika kikao cha Baraza.
Nae diwani wa kata ya Kwakilosa mheshimiwa Nzala Ryata amesema, baadhi ya sababu za kutohudhuria kikao hicho ni uwendeshwaji mbovu wa vikao vya baraza, kuwepo na hali ya upendeleo wa chama kimoja pamoja na kuwepo kwa hali ya mabavu wakati wa vikao.
Baraza la madiwani lilikuwa na lengo la kupitia agenda mbalimbali ikiwemo kuthibitisha agenda za mkutano wa baraza la madiwani wa tarehe 07.11.2018, pili maswali na majibu ya papo kwa papo kwa mujibu wa kanuni ya 24, kuthibitisha mihutasari ya mikutano ya Baraza la Madiwani ya tarehe 04.09.2018, 07.09.2018 na tarehe 21.09.2018, Taarifa za utekelezaji wa yatokanayo na mkutano wa Baraza la Madiwani wa tarehe 04.09.2018, Taarifa ya utekelezaji wa Maendeleo kwa kipindi cha ya robo ya kwanza (Julai – September,2018), Taarifa ya kudhibiti UKIMWI kwa kipindi cha robo ya kwanza (Julai – Septemba 2018), Kupokea taarifa, kuthibitisha muhutasari ya kamati za kudumu za Halmashauri ya Manispaa ya Iringa pamoja na maswaali na majibu kwa mujibu wa kanuni ya 23 pamoja na hoja binafsi kwaa mujibu wa kanuni ya 20.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa