Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ameipongeza Manispaa ya Iringa kwa kupata hati safi ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (C.A.G) kwa mwaka wa fedha 2017-2018.
Bi Amina Masenza ametoa pongezi hizo katika kikao cha Baraza maalum la Madiwani cha kupitia hoja za Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2017-2018 kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa ambapo hoja 41 zilijadiliwa na kupitiwa.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameutaka uongozi wa Manispaa kubuni vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza mapato ya ndani na kupunguza utegemezi wa Serikali kuu hasa katika kipindi hichi awamu ya tano.
Katika kikao hichi ameishauri Manispaa ya Iringa kuimarisha kitengo cha ukaguzi wa ndani ili kuongeza ufanisi wa kazi na kuepuka hoja.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa