Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amewaonya watu wanaoficha ushahidi wa vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuviagiza vyombo vinavyohusika kuwatambua na kuwafuatilia wale watakaokutwa na tabia hiyo.
Sendiga amesema hayo wakati wa kikao maalum baina yake na Waandishi wa habari kilichofanyika tarehe 23/9/2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Ameongeza kuwa watu wenye tabia hiyo hutoa maelezo polisi kuelezea vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini wanapotakiwa kutoa ushahidi mahakamani hupotea kwa kuwa huchagua kumalizana kifamilia.na hivyo kuwanyima haki waathirika wa vitendo hivyo na hata watuhumiwa.
Aidha amewaomba wanahabari kuendelea kuvifichua vitendo vya ukatili wa kijinsia bila kuchoka kwani wao ni wadau muhimu wa Serikali katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo na kwamba Mkoa utachukua hatua kila patakapohitajika.
Wakati huo huo Mh Sendiga amewakumbusha wananchi wa Mkoa wa Iringa umuhimu wa kuwapa watoto wao lishe bora ili kuchangia ukuaji wao; kwani Mkoa huo ni mmojawapo wa Mikoa ambayo inatajwa kuwa na udumavu unaosababishwa na lishe duni kwa watoto.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa