“Nitapita mtaa kwa mtaa kuwafuata wananchi waliko na kusikiliza kero zao, ziara hii nitaianza tarehe 21 katika Manispaa ya Iringa na nitatembea Mkoa mzima, wanaodhani kuwa Iringa mpya imeisha wajipange, lengo ni kuwafikia wananchi na kutatua kero zao huko waliko.”
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi alipotembelea wafanyabiashara wa soko kuu la Iringa na kufuatilia maagizo aliyoyatoa katika awamu ya kwanza ya Iringa mpya na kusikiliza kero zao.
Amesema wafanyabiashara wasibugudhiwe na wafanye biashara kwa uhuru kwani lengo la Mheshimiwa Rais ni kuwatengenezea wajasiriamali mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao.
Aidha ameuagiza uongozi wa SUMATRA katika Mkoa wa Iringa kuhakikisha ndani ya wiki tatu daladala zinaanza kupaki na kushusha abiria katika eneo hilo la soko ili kufanya mzunguko wa biashara kuongezeka.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo baada ya wafanya biashara katika soko hilo kulalamika kuhusu mzunguko wa biashara kuwa mdogo kutokana na kukosa wanunuzi katika eneo hilo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa