Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amesema ni vizuri jamii ikawa na utamaduni wa usafi endelevu ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na kuifanya Manispaa ya Iringa kuwa katika mazingira safi na salama
Sendiga ameyasema hayo leo eneo la mashine tatu mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika kwa ushirikiano mkubwa kati ya viongozi wa Serikali, Chama cha Mapinduzi na wafanyabiara ambapo alipata fursa ya kuongea na wananchi hao
"Usafi ni jukumu la kila mmoja wetu, usisubiri kuhimizwa kufanya usafi hivyo kila mmoja atimize wajibu wake na nimefurahi kuona mmejitokeza kwa wingi na mmeyatendea kazi maelekezo niliyowapa miezi mitatu iliyopita kwa sasa hali ya usafi inaridhisha alisema Sendiga
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Moyo ameagiza baadhi ya wafanya biashara kusafisha mitalo iliyo katika maeneo yao kwani imekuwa likisahaulika kusafishwa
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada ametoa onyo kwa wale wanaochukua vifaa vya kuwekea taka vilivyowekwa maeneo mbalimbali kwa lengo la kuweka mji safi kuacha mara moja tabia hiyo na kuwaagiza wafanyabiashara kuwa walinzi wa vifaa hivyo na kuwakamata watakaobainika kufanya hivyo
Awali akiongea na wajasiliamali Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Jesca Msambatavangu amewapongeza wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kufanya usafi amesema wao ni mfano wa kuigwa
Naye Katibu mkuu mtendaji wa wajasiriamali (machinga) Ndg. Joseph Mwanakijiji amesema wanawashukuru viongozi wote wa Manispaa na Mkoa kwani wamekuwa wakipata ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao na kuahidi kudumisha ushirikiano huo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa