Mkuu wa Wilaya ya Iringa ndugu Mohamed Moyo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika kata zote 18 Manispaa ya Iringa
'Natoa wiki moja kwa wakandarasi ambao hawajakamilisha ujenzi wa miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kukamilisha kazi hiyo mara moja ili miradi hiyo ianze kutumika kwa ustawi wa Manispa.'alisema Moyo
Moyo amesema Lengo la ziara hiyo ni kuangalia matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali na ubora wa miradi hiyo kama unaendana na fedha zilizotolewa
Aidha Moyo amewataka Wakandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo pia amesisitiza wazingatie ubora wa Miradi
Amempongeza Mkurugenzi kwa juhudi kubwa katika kusimamia miradi hiyo na kuwataka wananchi kuweka uzalendo mbele kwa kuitunza miradi kwani jukumu hilo la ulinzi ni la kwao
Omary Mkangama ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa amesema atayatendea kazi maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ikiwa ni pamoja na kufanya ukarabati mara moja katika majengo yaliyoharibika
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa choo zahanati ya kitanzini, kutembelea na kukagua shule ya Msingi
Azimio,ujenzi wa choo shule ya Msingi Chemchem na umaliziaji wa ujenzi wa jengo la Zahanati Itamba.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa