Mh. Richard Kasesela Mkuu wa Wilaya ya Iringa amezindua ujenzi wa madarasa sita katikashule ya Sekondari ya Tagamenda iliyopo Kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa kwa kuchimbaMsingi wa awali akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ndugu Omary Mkangama,Viongozi na wananchi wa Kata ya Ruaha pamoja Igumbilo ambazo zinaitumia shule hiyo kwakusomesha watoto wao.Uzinduzi huo umefunguliwa na bodi ya wazazi pamoja na Walimu siku ya ijumaa kimelengakuongeza maendeleo ya shule pamoja na kutatua changamoto mbalimbalizinazowakabili,changamoto kubwa ikiwa kubwa ni upungufu wa Madarasa 6 kutokana naongezeko la wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa asilimia kubwa ukilinganisha na mwaka jana.Akisoma taarifa hiyo Mkuu wa Shule ameelezea mafanikio makubwa walioyapata kitaarumaikiwa kupanda kwa ufaulu wa Kidato cha pili kwa asilimia 95% na kutoa A ya 7 kwa wanafunziwa tano ambao Mkuu wa Wilaya aliwazawadia elfu 20,000/= kila mmoja huku akitoa rai kwawalimu na wazazi kufuta F kwa matokeo ya Kidato cha nne 2018/19.Mwisho amemaliza kwa kuwapongeza Walimu kwa jitiada kubwa wanazozifanya shuleni apokitaaruma ikiwa ni pamoja nakuahidi kutatua changamoto zinginezo zinazo wakumba kamaujenzi wa Daraja na usafiri kwa wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali pia amewataka Wazaziwashirikiane na Walimu katika jukumu la malezi ya watoto kwa ujumla
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa