Walimu wakuu wa shule za Msingi na Sekondari kutoka wilaya za Mkoa wa Iringa ambazo ni Manispaa, Iringa Vijijini na Kilolo wametakiwa kutochezea maagizo yanayotolewa na Serikali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza alipokutana na walimu hao wakuu kufuatia kusimamia agizo lililotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli alilotoa tarehe 17/1/2018 kuhusu kuwaonya walimu kukusanya na kuchukua michango yoyote kutoka kwa wanafunzi.
Mbali na ayo Bi. Amina Masenza ametoa onyo kali kwa shule zinazowarudisha nyumbani wanafunzi ambao awajafikia wastani uliowekwa na shule hasa kwa shule za watu binafsi na kuwataka wawarudishe shuleni wanafunzi waliowafukuzwa kwani ni jukumu lao kuakikisha wamevuka wastani kwakua walishawapima kwenye usahili wa mwanzo na kujilizisha wanafaa kusoma shuleni hapo.
Amesisitiza kuwa ni marufuku kwa walimu kuwarudisha nyumbani wanafuzi kwa kukosa mchango, ada, kutokuwa na sare za shule na kutofikia wastani wa shule.Kikao hicho kimehudhuriwa na wakuu wa Wilaya wa wilaya za Kilolo na Iringa, wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na waratibu wa elimu kwa wilaya za Kilolo, Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa