Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameipongeza timu ya Mpira wa Miguu ya wanawake Mkoani Iringa MKWAWA QUEENS iliyofanya vizuri katika kufunzu na kuingia kwenye ligii kuu ya mpira wa wanawake Tanzania
Hayo ameyasema Septemba 24.2022 kwenye ukumbi wa shule ya wasichana ya Iringa, katika hafla fupi ya kuwapokea wachezaji wa timu hiyo kutokea Mkoani Dodoma ambapo ndipo yaliyofanyika mashindano ya kuwania kuingia Ligi kuu kwa mwaka 2022
Aidha katika ushiriki wao, timu hiyo ya Mkwawa Queens imetoa golikipa bora wa Mashindano pamoja na Mfungaji bora.
Sambqmba na mapokezi Mkuu wa Mkoa Mhe. Halima Dendego amewapa motisha ya kuwakabidhi kiasi cha shilingi laki moja kwa kila mchezaji na bechi la ufundi na akatoa ahadi ya kuwa pamoja nao kwa kila hatua ili kuhakikisha wanakuwa na timu bora itakayoleta ushindi lakini pia ameahidi kuwatafutia wadau ambao nao wataungana nae kuisimamia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri zaidi katika michuano iliyo mbele yao.
Awali akitoa taarifa kwa mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti Mkwawa Queens Ndg. Joel Musiba amesema timu hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo ni ukosefu wa mahala pazuri pakuishi wachezaji kwa maana ya hostel, Changamoto ya fedha kwa ajili ya kulipa mishahara pamoja na posho, pia upungufu wa vifaa vya michezo mfano mipira yakutosha
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa