Mjumbe Halmashauri kuu Taifa(Mnec) Ndugu Salim Abri Asas ameahidi fedha kiasi cha shilingi milioni 100 kwa wafanyabiashara wadogo (Machinga) lengo likiwa ni kuwasaidia kukuza mitaji yao na kufanya ujenzi wa vibanda vya kufanyia biashara.
Abri ametoa ahadi hiyo leo Machi 14 2023 katika uwanja wa Samora kwenye Mkutano wa dharula baina ya wafanyabiashara hao na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego ambao ulilenga kutatua baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa kuwapanga Machinga katika maeneo rasmi waliyotengewa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa ajili ya kufanyia biashara zao.
Natambua changamoto zenu wengine hamna vibanda vya kufanyia biashara na wengine hamna mitaji hivyo nitatoa shs milioni 100, ambapo shs milioni 50 zitumike kukuza mitaji yenu na 50 zitumike kujenga vibanda vya kufanyia biashara alisema Abri.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego amewataka Machinga kuwa watulivu na kuwahakikishia utaratibu mzuri wa kuwapanga ambapo yeye ndiye atasimamia zoezi hilo na kuhakikisha kila mfanyabiashara mdogo anapata eneo la kufanyia biashara.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahim Ngwada amemshukuru Mkuu wa Mkoa,Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa,Katibu wa CCM Mkoa,Secratarieti ya CCM jkwa jitihada kubwa walizozifanya za kutatua changamoto za wafanyabiadhara wadogowadogo.
Ngwada amesema Halmashauri imetenga fedha kiasi cha shs milioni 150 ambazo zitawanufaisha wafanyabiashara wadogo ambao watakaokidhi vigezo na kujiunga na SACCOS pia amesema Halmashauri imeanza ujenzi wa vyoo vitakavyotumika eneo hilo ambavyo vitatosheleza mahitaji ya wafanyabiashara hao.
Zoezi hilo la upangaji wa Machinga litaendelea tena Machi 15 2023 katika eneo la Soko la Amani Mwamwindi lililopo eneo la Mlandege na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa