Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini ndugu Hamid Njovu amewataka wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata na wilaya kuzingatia sheria,kanuni na taratibu kuelekea uchaguzi mkuu oktober mwaka huu.
Njovu ameyasema hayo katika kikao kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Iringa ikiwa ni maandalizi ya awali ya uchaguzi mkuu,amesema ni vizuri kutambuana na kujipanga katika zoezi linalokuja la utoaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na uteuzi.
Aidha Njovu amewataka wasimamizi wasaidizi kuepuka uharakati na uanasiasa kwa kuvaa mavazi ya chama fulani ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima pindi wanapotekeleza majukumu yao.
Pia amewataka kuchagua timu makini watakazofanya nazo kazi kwa weledi na kuzingatia muda uliowekwa kwa mujibu wa taratibu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa