Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini Ndg. Hamid Njovu amewataka mawakala wa uchaguzi kutoka vyama mbalimbali vya siasa kufuata sheria na taratibu za uchaguzi.
Ndg. Njovu ameyasema hayo hii leo wakati akiwaapisha mawakala hao na amesema ni wajibu kwa kila wakala kutunza siri za kituoni pia hawataruhusiwa kutumia simu, kamera au kinasa sauti wakati wa zoezi la upigaji kura.
"Sheria zetu za uchaguzi zimetaja hukumu iwapo utakiuka maagizo hayo kuwa ni faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi laki tatu au kifungo kisichopungua miezi sita au kuzidi miezi 12 au vyote kwa pamoja". Njovu alinukuliwa akiyasema hayo
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria wakala yoyote wa chama hatoruhusiwa kumsaidia mtu yeyote mwenye matatizo au asiyeweza kupiga kura mwenyewe hata kama ni ndugu yake kwani sheria inasema wazi nani atamsaidia na wakala atatakiwa kujaza fomu namba 14 ili kufahamu mwenendo mzima wa upigaji kura.
Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM tawi la Mtwivila Bw. Yohana Siha amesema jukumu kubwa kwa wao kama viongozi ni kuhakikisha amani na utulivu unatawala katika uchaguzi na kufuata taratibu zote na maelekezo ambayo tume inatoa.
Naye Edson Mahemba wakala kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA amewasihi viongozi watakao simamia uchaguzi kutenda haki kwa mujibu wa sheria na miongozo ya uchaguzi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa