Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwanda ametoa wito kwa wananchi wote kuzingatia usafi wa mazingira katika Maeneo yanayowazunguka
"Ni lazima tushike nafasi ya kwanza katika mashindano ya usafi yanayofanyika kila mwaka katika Halmashauri, Miji na Majiji kwani sioni sababu ya kushindwa kuchukua nafasi hiyo"
Ameyasema hayo Mhe. Ngwada siku ya Jumamosi tarehe 10/7/2021 katika eneo la Mashine tatu mara baada ya kufanya usafi katika maeneo mbalimbali yaliyopo Manispaa ya Iringa
Aidha Mhe. Ngwada amegawa vifaa vya kukusanyia taka 25 vyenye thamani ya shilingi 4,000,000/= ambavyo vimewekwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani, Soko kuu na maeneo ya barabarani ili vitumike kuhifadhia taka katika maeneo hayo kwa kuyafanya mazingira ya Manispaa kuwa safi
Kwa upande wake Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Jesca Msambatavangu akiambatana na Mstahiki Meya amewataka wananchi kutimiza wajibu wao katika kusafisha mazingira yao bila kusubiri kuhimizwa na viongozi kwani usafi unaanza na wao wenyewe na ni usalama wa afya zao
Ndg. Abdoni Mapunda ni Afisa Mazingira wa Manispaa ya Iringa, amesema vifaa vya kuhifadhia taka vitalindwa na wasimamizi wa maeneo husika ambao wamepewa funguo ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli hizo za usafi na utunzaji wa vifaa na kuongeza kuwa kutakuwepo na sheria ndogo zitakazotumika kwa wale watakao tupa taka hovyo
Ujio wa Vifaa hivyo vya kuhifadhia taka (durstbin) umeonekana kuwafurahisha wanachi na kuahidi kuvitumia kwa uangalifu ili viweze kuleta tija katika Manispaa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa