Mkurugenzi wa Halmashauri wa Manispaa ya Iringa Ndg. Kastory Msigala ameendelea na operesheni yake maarufu kama “Mtaa kwa Mtaa na Msigala” inayofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili kwa kutembelea viwanda na maduka makubwa kwa lengo la kuhakikisha wafanyabiashara wanamiliki leseni halali za biashara na wanalipa kodi mbalimbali kwa wakati ili kuikuza Manispaa ya Iringa.
Msigala ametembelea miradi mbalimbali ya ujenzi ili kuwakumbusha wasimamizi wa miradi hiyo ya Mabweni, Madarasa, Vyoo, Shule na Zahanati inakamilika kwa wakati na inajengwa kwa viwango vinavyotakiwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa