Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala amewataka watendaji wa Kata na Mitaa kutimiza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha Manispaa inapata Maendeleo.
Msigala ameyasema hayo katika muendelezo wa Ziara yake Maarufu kama MTAA KWA MTAA NA MSIGALA ambayo inafanyika kila Jumamosi na Jumapili akiambatana na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri kwa lengo la Kukagua leseni za biashara, Ushuru wa huduma (Service levy), Viwanda vikubwa na vidogo, Ushuru wa taka, Vibali vya ujenzi, Usafi wa mazingira katika mitaa na Ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri kwa fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu na mapato ya ndani.
“Watendaji nataka fedha za Halmashari mara moja au hatua mlizochukua kwao, kwasababu haiwezekani wafabiashara ni wengi na mapato yanayokusanywa serikalini hayaridhishi, nikawa najiuliza ni kwanini baadhi ya wafanyabiashara hawana leseni na wanafanya biashara?” amehoji Msigala alipokuwa ziarani Kata ya Kitwiru.
Akikagua miradi Msigala amewataka wataalamu kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo ili miradi hiyo iweze kutatua changamoto za wananchi.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari Kitwiru, Shule ya Msingi Kitwiru na Ujenzi wa nyumba ya mwalimu Isakalilo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa