MWENGE WA UHURU UMEKAGUA, KUTEMBELEA NA KUWEKA MAWE YA MSINGI KATIKA MIRADI 8 YA MAENDELEO ILIYOPO KATIKA KATA 7 MANISPAA YA IRINGA.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Mh,Charles Kabeho ameitaka timu ya Menejimenti Manispaa ya Iringa kufuatilia kwa ukaribu miradi mbalimbali inayotekelezwa ili kuimarisha ubora .
Kabeho ametoa agizo hilo katika mbio za mwenge Manispaa ya Iringa ambapo umekagua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi nane ya Manispaa ya Iringa, miradi iliyo tembelewa na mwenge wa uhuru ni pamoja na kuweka jiwe la Msingi mradi wa Maji Igumbilo- Kata ya Igumbilo, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa, Shule ya Sekondari Tagamenda-Kata ya Ruaha.kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara yenye kiwango cha rami Samora-Mashinetatu-Mkwawa-Kata ya Mwangata, Mlandege na Mkwawa. kukagua shughuli za kilimo cha kisasa (Greenhouse)-Kata ya Mkwawa, kukagua huduma za kituo kinachojihusisha na kupiga vita madawa ya kulevya- Kata ya Mtwivila, Kugawa vitambulisho vya matibabu bila malipo kwa wazee katika kituo cha afya ngome sambamba na ugawaji wa vyandarua- Kata ya Kihesa. Uzinduzi wa programu ya kupambana na rushwa kwa wanachuo wa chuo Kikuu Mkwawa pamoja na Kutoa mikopo kwa vikundi kumi vya vijana na wanawake- Eneo la Mkesha.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa