Mwenge wa uhuru kitaifa 2023 umeweka jiwe la msingi kwenye mradi wa kituo cha afya Itamba kilichopo Kata ya Mkwawa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa chenye thamani ya shilingi milioni.235,647,000/=.mradi ambao umetekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani.
Tukio hilo limefanyika leo tarehe 2.05.2023 mara baqda ya mapokezi makubwa na yaliyojaa shamra shamra katika Uwanja wa Shute ya msingi Kitwiru ambapo wananchi walijitokeza kwa wingi.
Akisoma tarifa ya mradi mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya iringa Dkt.Godfrey Mbangali amesema mradi huo utanufaisha wananchi wa vijiji...ambao watapata huduma za afya katika zahanati hiyo ambao awali walikuwa wanatembea umbali mrefu kwenda Hospitali ya Wilaya ya Frelimo.
Ndugu Abdalla Shaib Kaim kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa amesema amekqgua nyaraka zilizotumika kufanya manunuzi wakati wa ujenzi, kukagua jengo na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, pia amewataka wataalam kuwa makini wakati wa utekelezaji wa miradi ili iiendane na thamani ya fedha wanazotumia ikiwa ni pamoja na kukamilisha miradi kwa wakati.
Aidha Shaibu ameridhishwa na miradi yote sita (6) iliyokaguliwa.zinduliwa.kufunguliwa na mbio za Mwenge wa uhuru mwaka 2023.
Sambamba na hayo Kim amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na Taifa letu kama ambavyo kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema.
I metolewa na kaim mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa