Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Komredi Godfrey Mzava ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kukamilisha miradi 8 na kupitishwa na Mwenge wa Uhuru, ambapo amewaomba viongozi kuhakikisha wanasimamia kila mradi uliopitiwa ili huduma iliyokusudiwa na Serikali iweze kufika kwa jamii.
Ameyasema hayo katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru yaliyofanyika kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika Kijiji cha Muwimbi kilichopo Kata ya Lumuli.
Komredi Godfrey Mzava amesema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 zimeona na kukagua miradi iliyopangwa hivyo wameridhia na utekelezaji wa miradi yote 8 ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
"Tumeona ubora wa miradi, kwa ufupi Iringa Manispaa mmefanya kazi nzuri miradi tuliyoizindua muitunze na tuliyoiwekea mawe ya msingi ikamilike kwa wakati kwani mafanikio yote yaliyojitokeza ni kwa sababu ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Chama na Serikali, hivyo nawaomba muendelee hivyo hivyo, kwani penye ushirikiano pana mafanikio". Amesema Komredi Mzava.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Komred Kheri James amewashukuru Viongozi na Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, pamoja na wananchi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya tangu mapokezi ya Mwenge, na hatimaye kufikia zoezi la makabidhiano.
"Nakupongeza sana Mkurugenzi kwa kazi kubwa na nzuri pamoja na Madiwani chini ya usimamizi wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa na wananchi wote wa Iringa chini ya usimamizi wa Mbunge ambaye tumeshirikiana naye tangu mwanzo mpaka mwisho wa zoezi la kukimbiza Mwenge wa Uhuru, tuendeleeni kushikamana". Amesema Komredi Kheri.
Awali akiongea na wananchi muda mfupi kabla ya uzinduzi wa wodi ya wazazi Kituo cha Afya cha Itamba Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mheshimiwa Jesca Msambatavangu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za ujenzi wa miradi mbalimbali katika Sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu fedha ambazo zimechochea maendeleo katika Halmashauri yetu na Mkoa kwa ujumla.
#tume ya uchaguzi_TZ
#Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
#ofisiyawazirimkuu
www.kazi.go.tz
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa