Mwenge wa uhuru umezindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5
Akiongeq katika maeneo ya miradi leo tarehe 3/9/2022, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Sahili Nyanzabara amewataka wataalam wa ujenzi kufuata miongozo iliyowekwa na wizara wakati wa ujenzi wa miradi ili kuepuka kufanya kazi chini ya kiwango ama kinyume na miongozo hiyo
Nyanzabara amesema kutofuata maelekezo yaliyotolewa katika miongozo ni jambo ambalo halipaswi kuendelea kutokea vinginevyo wataalam wajitathmini katika eneo hilo .
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa uhuru mwaka 2022 katika Manispaq yaIringa ni Ujenzi wa jengo la madarasa mawili na ofisi moja, Ujenzi wa shule ya Sekondari Tagamenda,ujenzi wa shule ya mpya ya Sekondari ya Isakalilo, Ujenzi wa wodi mbili na jengo la upasuaji katika Hospitali ya Flerimo,Ujenzi wa barabara ya lami Mtwivila-Darajani- Ikonongo na ukaguzi wa vikundi vya ujasiliamali vya vijana na wanawake
Katika ziara hiyo mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa na kumshukuru kwa kukubali kuizindua na ,ameahidi kuyafanyia kazi mara moja,maelekezo yote yaliyotolewa na Kiongozi huyo.
Mhe Moyo amemshukuru Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi katika sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu katika Manispaa ya Iringa ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Jesca Msambatavangu ni Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini amewashukuru wataalam kwa kazi nzuri wanayofanya na kusisitiza matumizi mazuri ya rasilimali fedha zinazolewa na Serikali kwa manufaa ya umma.
Nyanzabara ametumia fursa hiyo kukemea vitendo vya rushwa,ameawakumbusha wananchi kuzingatia mlo kamili,kujikinga na malaria na kukemea vikali matumizi ya dawa za kulevya.
Aidha amewasisitiza wanachi kuhakikisha wanahesabiwa kwa maenfeleo na ya Taifa kwa ujumla.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa