Shirika lisilo la kiserikali la Mtandao wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (NACOPHA) kupitia Mradi wa 'hebu tuyajenge' umekabidhi pikipiki mbili katika Halmashauri mbili za wilaya ya Iringa .
Akizungunza Meneja wa mradi huo kanda ya Mbeya Ndugu. Ferdnand Mazuni amesema utolewaji wa pikipiki kama hizo, pia zimetolewa kwenye Halmashauri 15 nchini zinazotekeleza mradi huo.
Hata hivyo ameendelea kusema kuwa pikipiki hizo zitasaidia kwa watenda kazi kufuatilia mwenendo wa mradi huo.
"Kwa mwitikio wa mapambano dhidi ya UVICO 19 shirika hili limekabidhi vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona Kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI " alisema Ferdnand
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (KONGA), Halmashauri ya Iringa Ndg. Justin Mfilinge akishukuru Kwa msaada huo alisema kuwa vitendea kazi hivyo ni hatua kubwa ya Utekelezaji wa shughuli zao za kila siku na watahakikisha watavifanyia kazi kama inavyotakiwa.
Aidha katika maelezo yake kabla ya kupewa msaada wa pikipiki hizo wamekuwa na chanagamoto ya kutumia gharama zao binafsi katika kufuatilia taarifa kwenye Kata, ila sasa wataepuka gharama hizo.
Naye mratibu wa UKIMWI Tiba Katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dk. Godfrey Mtunzi alisema kuwa msaada huo umekuja wakati husika na kuwa itawasaidia katika mapambano dhidi ya UVICO 19.
Pia alisema vitakasa mikono vilivyotolewa pamoja na barakoa vitasaidia katika mapambano ya UVICO 19 Katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa hasa maeneo ya kwenye Kata.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Omary Mkangama amepongeza jitihada hizo za wadau hao katika mapambano dhidi ya UVICO 19 katika Halmashauri hiyo.
Vilevile alisema Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeendelea na mapambano ya UVICO 19 kwa kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na wataalam wa afya na kutaka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na kupata Chanjo ya UVICO 19 katika maeneo yote yanayotolea huduma hizo ikiwemo Ofisi zote za Kata.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa