Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa na Diwani wa Kata ya Kihesa Mhe.Julius Sawani amewaonya wananchi wanaotupa taka kwenye madampo yaliyotengwa maalumu kwa ajili ya masoko na badala yake wafuate utaratibu waliowekewa wa kutupa taka kwenye magari ya taka yanayopita mara mbili kwa wiki katika maeneo yao.
Akiongea na wananchi hao katika zoezi la uondoaji wa taka katika dampo la soko la Ngome-Kihesa Mhe.Sawani amesema kuwa wananchi wachangie gharama za ukusanyaji wa taka katika maeneo yao, na sio kuipa Halmashauri mzigo wa kuondoa taka wanazotupa katika madampo.
"Tumerudi kwenye utaratibu, kila Kaya inatakiwa ichangie Shilingi elfu moja kwa ajili ya gari la ukusanyaji taka linalopita kwenye maeneo ya mitaa hivyo utaratibu wa kuweka taka kwenye kontena au madampo ni kwa ajili ya masoko, hospitali na kwenye mashuleā€¯Aamesema Sawani
Aidha Sawani amesema kuwa Halmashauri inafanya jitihada kubwa kuzingatia usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Iringa, tatizo linajitokeza kwa baadhi ya wananchi kutokuwa na elimu au kutochangia gharama za uzoaji taka na kupelekea kutupa taka maeneo yasiyo rasmi kama vile kwenye madampo ya masoko' mashuleni hivyo kuleta adha ya uchafuzi wa mazingira.
Sawani ameshauri kuwa Watendajii wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Miitaa watoe elimu juu ya uchangiaji wa gharama za uzoaji taka, pia kuwekwe mabango ya onyo kwa mwananchi yeyote atakayebainika kumwaga taka maeneo yasiyoruhusiwa achukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.
Aurelia Sanga ni Mfanyabiashara katika Soko la Ngome anakiri kuwepo kwa mabadiliko makubwa kwani awali eneo lilikiwa haliridhishi na kuhatarisha afya ya wauzaji pamoja na wateja lakini tangu oparlationi hiyo ianze Soko limekuwa safi na wanafanya biashara kwa utulivu.
Oparationi ya usafi kwa kuondoa taka katika madampo yote kwenye maeneo ya masoko yaliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni endelevu ambayo imeanza mwishoni mwa wiki iliyopita kuanzia Soko la Ngome- Kihesa ambalo imesimamiwa na Maafisa wa afya na Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa