Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Mhe.Mwanaid Khamis ametoa agizo kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwapatia eneo kwa ajili ya matumizi ya kituo Shirika la Daily bread life kilichopo kata ya Gangilonga ili kutatua changamoto ya ufinyu wa eneo inayowakabili
Akitoa agizo hilo katika ziara yake iliyofanyika tarehe 8/7/2021 Mhe.Khamis amesema kuwa anawapongeza walezi wa watoto waishio katika kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kurekebisha tabia za watoto waliopo hapo.
Aidha Mhe. Khamis amesema Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania inawapenda na kuwajali watoto hivyo inamipango mizuri ya kuhakikisha watoto wanapata haki zao wanazostahili na ameahidi kushirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha anatatua changamoto zote zilizopo.
Neema Mpeli ni Mkurugenzi wa Daily bread life amesema Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kushirikiana na Shirika hilo ilianza kutekeleza mpango wa marekebisho ya tabia April 2020 na mpaka sasa kuna watoto 50 ambao wamepata huduma ya marekebisho ya tabia,watoto 9 kati yao tayari wamehitimu.
Bi. Mpeli amesema pamoja na mambo mengine pia Shirika linatoa huduma mbalimbali kama ushauri nasaha na elimu ya ujasiriamali lengo likiwa ni kubadili tabia za vijana waliokinzana na sheria
Naye Kaimu Mkurugenzi Bi. Mwantum Dossi alimshukuru mgeni rasmi kwa zawadi alizotoa katika shirika ambazo ni Michele gunia 3 kama mchango wake wa upendo kwa watoto waishio kituoni hapo na kuahidi kutekeleza maagizo yote aliyoyatoa kwa Manispaa
Ziara hiyo ilikamilishwa kwa kutembelea shughuli zinazofanywa na watoto waliopo kituoni ambazo ni bustani za mbogamboga, uokaji wa vitafunwa na utengenezaji vifungashio
Ester Kibiki ni mzazi wa mtoto aliyepata huduma anatoa ushuhuda wa namna ambavyo mtoto wake amenufaika kwa kipindi kifupi na amejifunza mambo mengi ambayo yamebadilisha tabia yake na kupanua uelewa na amewashukuru walezi kwa jitihada wanazofanya kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa watoto
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa