Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angeline Mabula amefanya ziara na amekutana kuzungumza na Wakurugenzi pamoja na watumishi wa Ardhi Mkoani Iringa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugalo iliyopo Manispaa ya Iringa tarehe 26.02.2021
Akizungumza na hadhara hiyo Mhe. Mabula amesema, dhumuni la ujio wake ni kukagua na kuhamasisha juu ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali ambapo Mkoa wa Iringa mpaka sasa umefanikiwa kukusanya kwa asilimia 48
"Jukumu la ukusanyaji wa kodi za ardhi ni letu sote, hivyo tuhakikishe tunawajibika katika hili lakini pia niwaombe wale wadaiwa sugu kulipa madeni yenu maana mnafanya shuguli zingine za kiserikali kutokamilika kwa wakati" Mhe.Mabula aliongezea
Aidha kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoani Iringa Ndg. Wenslaus Mtui amesema kwa kiasi kikubwa tangu kuanzishwa kwa Ofisi za Ardhi Mkoa wa Iringa zimesaidia kupunguza migogoro mingi ya Ardhi kwa wananchi hali ambayo hapo mwanzo ilikuwa ni changamoto kwakuwa Ofisi zilikuwa Mbeya katika ukanda wa kusini mwa Tanzania
Akiwasilisha tarifa yake ya Mkoa ndugu Mtui katika utendaji kazi amesema kwa sasa Mkoa wa Iringa katika Sekta ya ardhi kuna changamoto ya upungufu wa watumishi hali inayopelekea kushindwa kufanya kazi kwa uharaka na kwa wakati huku akisema vitendea kazi pia ni changamoto
Naye, Mhe. Richard Kasesera, Mkuu wa Wilaya ya Iringa ameipongeza Serikali kwa ufunguzi wa Ofisi hiyo huku akitaja kuwa changamoto ya elimu kwa wananchi ni moja ya kikwazo cha ulipaji wa kodi ya Ardhi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa