Naibu Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhe. Mhandisi Stella Manyanya amekutana na wanafanya biashara wa Manispaa ya Iringa na kuahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili ili kuendana na kasi ya viwanda inayoendelea nchini.
Akizungumza na Wafanyabiashara hao katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo naibu waziri ameziagiza Taasisi za serikali ikiwamo TRA na TANESCO kua na ushirikiano mzuri wa kiutendaji na sekta binafsi hususani wafanya biashara wa viwanda vilivyopo ndani ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha wanapata Umeme wakutosha maeneo yaliotengwa kwaajiri ya Viwanda na pia kupunguza gharama za kodi zilizo zidi kwa upande wa TRA jambo ambalo litachangia kukua kwa kasi katika biashara na kuvutia wawekezaji wengi ndani ya Manispaa ya Iringa.
Mwisho naibu waziri amehitimisha kwa kuwashukuru wafanyabiashara kwa kuitikia wito kwani ujio wao ni ishara tosha ya uhusiano mzuri na urafiki kati ya Serikali na sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa taifa ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2020/2025 pia amewasisitiza wafanyabiashara ndani ya Manispaa ya Iringa wasiogope kufika ofisi za Mkuu wa Wilaya kuzungumza nae endapo kutatokea tatizo baina yao na serikali kiutendaji.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa