"Muwe makini katika malezi ya watoto wetu kwani taifa linawategemea hasa katika kuwaepusha na ukatili dhidi yao. Hivyo tujitahidi kutoa Elimu ushauri hata mapendekezo Ili kuona maisha ya watoto wetu na wanawake ni ya amani na furaha"
Kauli hiyo imezungumzwa na Hamid Njovu, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa katika ufunguzi wa Semina ya Wenyeviti wa Mitaa iliyoandaliwa na Ofisi ya Ustawi wa Jamii Manispaa kwa kushirikiana na dawati la Jinsia.
Aidha semina hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa HallFare ikiwa na lengo la kutoa Elimu kwa wenyeviti hao juu ya ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto.
Sambamba na hilo, wawezeshaji mbalimbali walipata nafasi ya kuzungumza mada zilizohusu namna ya kuwasaidia kutokomeza ukatili wa watoto na wanawake huku wakihimizwa kutambua viashiria mbalimbali vya matukio ya unyanyasaji dhidi ya makundi hayo na kuyatolea taarifa mara moja yanapoonekana.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa