Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia Ofisi ya Maendeleo ya Jamii imewakabidhi mkopo wa shilingi Milioni 162 kwa vikundi vya wanawake 51, vijana vikundi 26 pamoja na walemavu vikundi vi 5 nakufanya jumla ya makundi 82 ya wanufaika
Tukio hilo limefanyika leo tarehe 24.06.2021 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri huku mafunzo mbalimbali ya matumizi ya mkopo yakitolewa kwa wanufaika hao kutoka kwa wadau wa fedha (benki ya NMB) na wataalamu wa Manispaa
"Niwapongeze kwa kupata mkopo na niwaombe kuwa waaminifu katika marejesho na hakikisheni mnaenda kuifanyia kazi kama mlivyoiombea"
Hayo yamezungumzwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Iringa Ndg. Mwantumu Dosi akiwa ni mgeni rasmi katika kufungua mafunzo hayo na kukabidhi fedha hizo
Kwa upande wake Ndg. Dora Myinga ambaye pia ni Afisa maendeleo ya Jamii amewaasa wanufaika kuzingatia kulinda afya zao dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI pia kupambana dhidi ya udumavu na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Abdala Mwaipopo mmoja wa wanufaika wa mkopo huo amemshukuru Mkurugenzi kupitia ofisi ya Maendeleo ya jamii kuwapatia mkopo huo na kuahidi kuufanyia kazi ipasavyo na kuurejesha kwa uaminifu na kwa muda waliopangiwa
Akihitimisha kikao hicho Ndg. Dossi amewataka wanufaika hao kufika ofisini kwake endapo watapata changamoto yoyote.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa