“Nawaombeni sana viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania Pamoja na viongozi wote. Pili, katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi nawaomba mzidi kuhubiri juu ya amani, na utulivu huku mkikemea matendo yoyote yenyekuleta tafaruku ikiwemo rushwa kwakuwa tunahitaji kupata viongozi bora na sio bora viongozi”
Kauli hiyo imesemwa na Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya Nne, Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda katika mkutano wake na viongozi mbalimbali wa Dini, uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mkoa (Iringa), dhamira ikiwa ni kuwaomba wajitahidi kuliombea Taifa hasa katika kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Aidha Mh. Pinda aliwataka viongozi hao wazidi kuonesha ushirikiano kwa Serikali kama ilivyo awali kwa kukemea baadhi ya mambo yatakayoleta mivurugano ikiwemo rushwa kutoka kwa wagombea.
Ikumbukwe kuwa kiongozi huyo alipofika Iringa kabla ya mkutano huo, aliweza kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa lengo ikiwa ni kuangalia utendaji kazi wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka 5 katika awamu ya kwanza ya Raisi Magufuli.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa