Katibu tawala wa Mkoa wa Iringa, Bi. Happiness Seneda jana alifanya kikao na watumishi wa Manispaa ya Iringa na kuzungumza nao masuala mbalimbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero zao.
Akizungumza katika kikao hicho Bi. Happiness amewataka watumishi hao kujitahidi kuepukana na rushwa, kujitoa zaidi kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi na kudumisha umoja na upendo baina yao.
Aidha Bi. Happiness amewashauri watumishi hao kupata muda wa kupumzika na kujali afya zao kama moja ya njia itayowafanya kuwa vizuri katika utendaji kazi yao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa