Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego ameshuhudia uwekaji saini wa maridhiano baina ya viongozi wa Umoja wa madereva Bajaji,Daladala na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa yaliyofanyika julai 13 2023 katika ukumbi wa RAS, wakiongozwa na mwanasheria wa Mnispaa ya Iringa Ndugu Nicholaus Mwakasungura.
Maridhiano hayo yamefanyika kwa lengo la kuwezesha Bajaji na Daladala kutoingiliana katika njia zao za kusafirisha abiria(route) na wafanye shughuli zao kwa utulivu.
Akizungumza mara baada ya tukio hilo kukamilika Mhe. Dendego ameutaka uongozi wa Umoja wa madereva Bajaji kuyaheshimu na kutii maridhiano hayo ili kuepusha migogoro isiyo kuwa ya lazima.
"Hakikisheni haya Maridhiano yanafatwa kwa vitendo, sitegemei tena kuona Bajaji mnawaingilia Daladala kwenye njia zao, naomba hili lisijitokeze tena, fateni taratibu ili kila mtu afanye kazi zake za kutafuta riziki kwa haki na ufasaha, Alisema Dendego"
Mwanasheria wa Manispaa ndugu.Nicholaus Mwakasungura amesema Maridhiano hayo walipewa siku moja kabla wakasoma na kuelewa hivyo wanasaini kitu wanachokielewa vizuri.
Naye Ndugu Titus Kihwele Mwenyekiti wa Umoja wa madereva Bajaji amesema ameridhika na maridhiano hayo na kuwa hana taarifa zozote zakuhusiana na umoja huo kujipanga kugoma, na haiwezi kutokea kugoma isipokuwa kuhusuana na faini ya kuanzia Tshs. 200,000 hadi 1,000,000 ni kubwa hivyo atafata utaratibu wa kukaa na viongozi wanaohusika kuona namna ya kupunguziwa faini hiyo ambayo ni kubwa ukilinganisha na kipato chao.
Katibu wa Madereva wa Daladala ndugu Fadhili Maluzuku amesema ameridhika na maridhiano hayo lakini ameomba Halmashauri kutoipunguza faini ili kuongeza umakini kwa madereva Bajaji ambao wanavunja sheria na taratibu zilizowekwa na anaamini faini hiyo inalenga kujenga tabia ya kutokiuka sheria ndogo zilizowekwa na Halmashauri na si vinginevyo.
Afisa Mfawidhi LATRA Iringa Ndugu Joseph Umuti amesema kwa sasa kuna Bajaji zaidi ya 1800 na hawataendelea na usajili wa Bajaji zilizotumika toka nje ya Mkoa wa Iringa kutokana na udogo wa Mji wa Manispaa na hali ilivyo kwa sasa ambapo bajaji zimekuwa zikiongezeka idadi kwa kasi siku hadi siku.
Imetolewa na
K/ Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Mamispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa