Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi itakayo kaguliwa,zinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru septemba 3. 2022 katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Dendego ameridhishwa na miradi iliyochaguliwa na wataalam na ameitaka Menejimenti ya Manispaa ya Iringa kufanya maboresho madogo madogo ya miundombinu katika maeneo yatakayopitiwa na Mwenge wa uhuru ili kusiwepo na dosari katika ugeni huo wa Kitaifa.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa ndugu Gerald Mwamuhamila amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa na kuahidi kuyafanyia kazi mara moja.
Ziara hiyo ya siku moja imefanyika leo tarehe 27/8/2022 ikiwa zimebaki siku chache Mwenge wa uhuru kuwasili katika Mkoa wa Iringa ambapo Manispaa ya Iringa Mwenge utakagua,utazindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi minne(4)ya Maendeleo.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Madarasa mawili na Ofisi Shule ya Sekondari Tagamenda,ujenzi wa Shule ya Sekondari ya kisasa(SEQUIP) Isakalilo na Ujenzi wa Majengo mawili ya wodi za upasuaji Hospitali ya Flerimo.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Moyo,kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na Wilaya ikiwa na lengo la kujiridhisha na maandalizi yaliyofanywa na Manispaa kwa ajili ya ujio wa Mwenge wa uhuru.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa