Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ally Hapi, amefanya ziara ya Kutembelea,kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye baadhi ya miradi iliyopo Halimashauri ya Manispaa ya Iringa.
Miradi iliyowekwa mawe ya msingi ni mradi wa shule mpya ya sekondari ya Igumbilo pamoja na mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala stendi kuu ya Igumbilo.
Hapi amefurahishwa na usimamizi mzuri wa Mkuu wa wilaya Richard kasesela na Mkurugenzi Hamid Njovu kwa hatua hiyo kubwa na nzuri iliyofikiwa kwani kukamilika kwa miradi hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi pia kuimarika kwa uchumi wa Halmashauri kutokana na ongezeko la mapotato yatakayotokna na Hoteli iliyopo ndani ya stendi ya igumbilo.
Wakati huohuo Mkuu wa Mkoa wa Iringa ametembelea na kukagua ukarabati katika shule ya sekondari lugalo na ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari Iringa girls na kuongea na wanafunzi wa shule hizo ambapo amewataka kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.John pombe Magufuli kwa kutambua umuhimu wa Elimu bora amewajali na kuamua kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu ili kuboresha sekta ya Elimu Mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Hapi amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa imemalizika kwa kuhutubia wananchi katika eneo la Mkimbizi kwa Shayo kata ya kihesa mara baada ya mkuu wa Mkoa kuhutubia wananchi na kusikiliza kero zao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa