Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga, amesema kwa sasa hakuna mpango wa kuhamisha makaburi ya Mlandege kwa mlengo wa kuwahamishia wajasiriamali kufanya biashara katika eneo hilo
Hayo ameyasema leo alipohudhuria mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa la kupitisha mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa
Aidha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amesema pamekuwepo na hali ya kutoelewana baina Madiwani wenyewe lakini pia baina yake na wajasiriamali
Mhe. Ngwada amesema "suala hili limeleta mgawanyiko baina yetu sisi madiwani pamoja na maneno kwa wajasiriamali kuwa mimi ndio nakataa kuhamishwa kwa makaburi ya Mlandege na kuwa eneo la wajasiriamali”
Sambamba na hilo RC Sendiga amesema amefanikiwa kuzungumza na viongozi wa BAKWATA pamoja na wazee wa mila juu ya swala hilo na kuwaomba wao pamoja na madiwani hao kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwatenga machinga kwenye maeneo husika na kuwaomba kama itafikia hatua ya kutaka makaburi hayo kuhamishwa basi taratibu zote za zitafatwa kuanzia ngazi ya chini
“hoja za msingi zitakapokuja na taratibu zikifatwa basi makaburi yatahamishwa kama sheria itakavyo wataka hivyo sioni haja ya kuweka migogoro isiyo ya lazima na kuacha kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa kuwaletea maendeleo” Mhe. Queen amesema
Mwisho Mkuu wa Mkoa amewataka Madiwani hao kumsaidia kutunza utulivu wa jambo hilo, Amani na kutekeleza maelekezo ya Rais kwa kuwapanga wajasiriamali na kama kutakuwa na jambo lolote wafike ofisini kwake kwa mazungumzo ya kina Zaidi na sio kukimbilia katika vyombo vya habari na kuzungumza bila kuwa na taarifa za uhalisia
Naye Meya akamshukuru RC kwa kuitikia wito huo na kwa majibu aliyoyatoa kuhusu suala hilo
“Niwaombe Madiwani wenzangu mjadala wa makaburi uiishe kuanzia leo na tuendelee kushirikiana vyema katika kuwatumikia wannchi kuleta maendeleo katika Manispaa yetu” Mhe. Ngwada alimalizia kwa kusema hayo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa