"Hakikisheni watoto wenu wanapatiwa chanjo hii ya polio kwani itawakinga dhidi ya kupooza au hata kupoteza maisha"
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga leo katika uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya chanjo ya matone ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5
Aidha Mhe. Queen Sendiga amesema kwa awamu hii wanadhamiria kuwafikia watoto zaidi ya Elfu 68 ambao wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo
"Nitoe wito kwa wataalamu kuimarisha kampeni na utoaji wa huduma hii kwa ubora mkizingatia elimu mliyopewa ya jinsi mnavyotakiwa kuifanya" Mhe. Queen Sendiga aliongezea
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa polio kwani unaweza kuwapata watu wenye umri wowote
Aidha ameishukuru Ofisi ya TAMISEMI na Wizara ya Afya kwa kuandaa kampeni hii kwani itasaidia kuboresha afya za watoto na kuwaandaa vijana wapambanaji wa taifa la kesho.
Pia katika ufunguzi wa kampeni hiyo ameongozana na viongozi wengine wa serikali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Happiness Seneda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo amesema anaahidi kufatilia vyema uendeshwaji wa zoezi hili na amewataka wataalamu wanaoshughulika nalo kuhakikisha wanatoa ripoti ya kazi kila siku mara baada ya zoezi kuhitimishwa
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa